KANISA ANGLIKANA TANZANIA DAYOSISI YA VICTORIA NYANZA

  • Home
  • About Us
  • News Updates
  • Events
  • Contact Us
  • Login Panel
    • Staff Login
    • Admin Login
  1. Home
  2. UMAKI

IDARA YA WANAWAKE (UMAKI)


Rose Malugu
MRATIBU UMAKI – DVN

Utangulizi

UMAKI – Maana yake ni Ushirika wa Wamama wa Kikristo, Idara ya UMAKI kazi yake ni kusimamia utekelezaji wamipango yote ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiroho katika jamii, UMAKI inafanya kazi kwa kushirikiana na Parishi zote na makanisa madogo. Pia UMAKI ni chombo cha Kanisa Anglikana Tanzania. Walengwa ni wanawake wote kuanzia ngazi ya tawi mpaka Dayosisi.

DIRA

Ni kuwa na jamii yenye maendeleo kiuchumi inayomjua Mungu na inayopata huduma zote za kiroho na kijamii.

DHAMIRA

UMAKI inadhamira ya kutoa huduma za kiroho na kulitambulisha Kanisa katika jamii. UMAKI inaratibu shughuli za maendeleo ya kiuchumi kwa kutoa Elimu ya miradi kwa wanawake kwa kutumia rasilimali zinazo wazunguka kwa lengo la kujenga jamii yenye mabadiliko chanya kiroho na kimwili.

DHUMUNI LA UMAKI

Kuwajengea wanawake uwezo na familiya zaokatika kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo kiroho na kimwili .

MALENGO YA IDARA YA UMAKI

1. Kuwafikia wanawake wote kwa Elimu ya neno la Mungu ili kulifanya kanisa kukua na kuongezeka.
2. Kutoa huduma kwa wahitaji kwa kuzingatia mahitaji ya kiroho na kimwili, kwa wagonjwa , mahospitalini wajane na watoto yatima na kuwatia moyo wazazi katika malezi ya watoto.
3. Kuwa na miradi endelevu na shirikishi toka ngazi ya Kanisa hadi ngazi ya dayosisi.
4. UMAKI kuendelea kutoa Elimu kwa wanawake katika makanisa ili kuwajengea uwezo wa kuanzisha shughuli ndogondogo za kujipatia kipato Mf.ujasiliamali.
5. UMAKI inaimarishwa na makusudi matano (5) ambayo msingi wake ni maandiko matakatifu kwaajili ya kugusa maisha ya watu kiroho na kimwili yaani huduma timilifu. (A wholistic ministry).

UONGOZI WA UMAKI – DVN

1. MARY NTUNZA : MSHAURI
2. GHATI CHACHA : M/KITI
3. RUTH Y. MSIMBA : M.M/KITI
4. NSIA MUSHI : MHAZINI
5. ROSE MALUGU : MRATIBU

Quick Links


  • Nyumbani
  • Isamilo International school
  • Kuhusu Sisi
  • Matukio Yote
  • Habari Mpya
  • Wasiliana Nasi
  • Build Project
  • Chuo cha Biblia Nyakato


Idara Mbalimbali

  • Idara ya Uhasibu
  • Ugavi na Manunuzi
  • Uinjilisti
  • Elimu
  • Vijana(TAYO)
  • Wanawake(UMAKI)
  • Watoto(SUNDAY SCHOOL)

Mawasiliano Zaidi

+255-759797219
+255-756435471
victorianyanza@yahoo.com

©Dayosisi ya Victoria Nyanza. Haki zote Zimehifadhiwa||Designed and Developed by DVN TAYO Ilemela 2025