TAYO – Maana yake ni (Tanzania Anglican
Youth Organisation)
DIRA
Huduma bora kwa Vijana wa Kanisa la Anglikana
Tanzania Kiroho na Kimwili
DHAMIRA
Kuwa na Vijana waliokomaa kiroho, kiakili kimaono kwa ajili ya uendelevu wa Kanisa na jamii
MADHUMUNI YA TAYO
•Kuilinda na kuitunza Imani ya Kikristo.
•Kufanya uinjilisti, kwa kutumia vipawa tulivyopewa na
Mungu kwa utukufu wa jina lake.
•Kuratibu na kusimamia shughuli zote za TAYO.
•Kuimarisha Amani, Upendo, na heshima kwa Vijana wote.
•Kushirikiana na Vijana wengine duniani.
•Kuboresha Afya ya uzazi, kwa kutafuta elimu sahihi ya
maisha na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa
UANACHAMA
•Mkristo aliye na umri kati ya miaka 13-40.
•kristo aliyezidi miaka 40 anaweza kuendelea na
uanachama isipokuwa hawezi kushika nafasi ya uongozi wa
TAYO.
•Umoja wa vijana katika madayosisi yote watakuwa
wanachama wa TAYO.
•Jumuiya nyingine zitakazokubaliana na muongozo huu.