Idara ya uhasibu ni kitengo kinachosimamia masuala yote ya Fedha za Dayosisi kwa mwongozo wa sera ya Fedha, sera ya Utumishi na taratibu maalum za hesabu.
DIRA
Kuwa kitengo cha kuaminika na madhubuti katika kulinda Fedha za Dayosisi na kudumisha uwazi na umakini katika kutoa huduma.
DHAMIRA
Kuratibu na kusimamia kwa usahihi Fedha zinazoingia na kutoka kwa Dayosisi na Parishi.
KAZI ZA IDARA YA UHASIBU
• Kuandaa bajeti ya mutumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo ya kila mwaka.
• Kufuatilia na kushauri kuhusu bajeti ya matumizi ya Dayosisi.
• Kutayarisha taarifa za Fedha za robo mwaka na mwisho wa mwaka.
• Kusimamia ukaguzi wa taarifa za fedha za kila Idara na Parishi.
• Kuhakikisha kwamba mapato yote ya Dayosisi yanakusanywa ipasavyo na kupelekwa Benki.
• Kulipa madai kwa wakati.
• Kuweka utaratibu wa kulinda Fedha za Dayosisi.
• Kusaidia shughuli zote zinazohusu ustawi wa wafanyakazi wa DVN.
• Kufanya kazi zote kama atakavyoelekezwa /agizwa na katibu wa Dayosisi.
Wafuatao ni wajumbe wa kamati ya Fedha ya Dayosisi
1. +RT. ZEPHANI AMOSI NTUNZA - ASKOFU
2. BEATRICE MALIFIMBO - MWENYEKITI
3. LILIANI JULIUS BOMBE - KATIBU
4. CAN. REV. JOSEPH KITWE - VICAR GENERAL
5. CAN. REV. KEPHA MLUGU - KATIBU WA DAYOSISI
6. GODFREY ELIAS SINYAGWE - MJUMBE
7. ABEL DENDWA - MJUMBE
8. ALLAN CHIPALO - MKAGUZI WA NDANI